Friday, July 11, 2014

BONDIA FRANCIS CHEKA APANDISHWA MAHAKAMANI KUJIBU MASHITAKA YA KUMPIGA NA KUMJERUHI MENEJA WAKE WA BAA.


Cheka akiwa chini ya Ulinzi Mkali Mahakamani


Bondia Francis Bonifas Cheka amepandishwa kizimbani leo katika mahakamani ya hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Morogoro  kwa mara ya kwanza na kusomewa shitaka la shambulio la kumpiga  na kumjeruhi aliyekuwa meneja wa baa yake.

Akisoma mashitaka mbele ya hakimu wa mahakama ya mkoa wa Morogoro Saidi Msuya mwendesha mashitaka Aminata Mazengo amesema julai 02 mwaka huu Cheka bila halali na huku akijua ni kosa  kisheria kifungu namba 241 cha makosa ya jinai alimpiga ngumi Bahati Kabanda kichwani na tumboni na kumsabishia maumivu makali.

Bondia Francis Cheka Akiwa na  Mikanda yake      

Meneja wa Baa ya Vijana Social hall Bahati Kabanda iliyechezea kichapo kutoka kwa Bondia Francis Cheka

Cheka ambaye ni Bondia wa ngumi za kulipwa namba moja nchini na anayeshikilia mkanda wa WBF, inadaiwa kumpiga meneja wake wa baa baada ya meneja huyo kushindwa kumkabidhi hela inayopatika katika baa hiyo hali iliyopelekea bondia huyo kumshushia kipigo.

Waandishi wa Habari nao hawakuwa nyuma kufuatilia tukio hilo
 
 
  Mtuhumiwa katika kesi hiyo amekana mashtaka na Kesi  hiyo imehairishwa na inatarajia kusikilizwa tena julai 23 huku Cheka akiachiwa kwa dhamana baada ya Mahakama kutoa masharti ya dhamana, ikimtaka Mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja kuweka dhamana ya maandishi ya shilingi milioni moja ambayo ilitimizwa.


No comments:

Post a Comment