Friday, May 27, 2016

LIGI YA WANAWAKE NA U20 KUDHAMINIWA NA AZAM MEDIA KWA MSIMU WA 2016/2017




Kampuni ya Azam Media LTD na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wamesaini Mkataba wenye thamani ya shilingi Bilioni Mbili wa kurusha Matangazo ya moja Kwa moja ya Mechi za Ligi Kuu ya Vilabu vya Wanawake nchini (Tanzania Women Premier League) na U20.


Mkataba huo ni wa miaka mitano ambapo Ligi Kuu ya Vilabu vya Wanawake itaanza kwa kushirikisha vilabu 10 na Ligi ya U20 itashirikisha vilabu vyote vya Ligi Kuu.

Kila Klabu ya Ligi Kuu itawajibika kuwa na timu ya U20 Kama ilivyo ada kanuni za uendeshaji wa mashindano haya zitatungwa na TFF na Ligi hizo zitaanza msimu wa mwaka 2016/2017.


Wanawake wapenda michezo sasa kazi ni kwenu, nafasi ndio hiyo itumieni kuonyesha vipaji vyenu hili tuwe na timu ya taifa imara na yenye kuleta upinzani na siyo kushiriki tu.

MWISHO:

No comments:

Post a Comment