Monday, May 16, 2016

MKENYA ATIWA MBARONI KWA KUDANDIA HELKOPTA....






SALEH WANJALA, akiwa na majeraha baada ya kuruka kutoka kwenye ndege






























Mtu huyo anaitwa Saleh Wanjala ambaye hakutoa sababu za kufanya hivyo, alishikiliwa na Jeshi la polisi huku akipata matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa Bungoma.

Wanjala alionekana akining’inia kwenye helikopta iliyobeba mwili wa mfanyabiashara Juma wakati ikipaa kutoka kwenye Uwanja wa Posta mjini Bungoma baada ya wananchi kutoa heshima za mwisho.

Wanjala aliamua kuidandia helikopta hiyo wakati ikiondoka kupeleka mwili wa mfanyabiashara huyo nyumbani kwake katika Kijiji cha Mungore.

Akisimulia mkasa huo, Wanjala alisema alikuwa karibu na helikopta hiyo wakati ikianza kupaa na kwamba aliumia baada ya mguu wake kukwama.

“Nilikuwa nimeketi chini ya helikopta na wakati ilipokuwa inaanza kupaa, mguu wangu ulikwama hapo ikabidi nijishikilie vizuri ili nisianguke,”alisema Wanjala.

WATU WaKIWA WAMEDUWAA WAKIMUANGALIA SALEH WANJARA AKIWA AMEDANDIA NDEGE
Rubani wa helikopta hiyo alilazimika kumpeleka hadi uwanja wa ndege wa Bungoma mita 700 kutoka kwenye uwanja huo lakini Wanjala aliamua kuruka na kuumia vibaya miguu na mikono. Muuguzi wa Hospitali ya Bungoma, Leah Atsewa alisema bado wanamfanyia uchunguzi. 


No comments:

Post a Comment