Mwamuzi mahiri nchini, Israel Mujuni Nkongo wa Dar es Salaam, Jumatano Mei 25, 2016 ameteuliwa kuwa mwamuzi atakayechezesha mchezo wa fainali za Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) mchezo utakaozikutanisha timu za Young Africans na Azam FC zote za jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo utakaochezwa katika uwanja wa Taifa Dar es salaam utaanza majira ya saa 10.30 jioni, huku waamuzi wasaidizi watakuwa Ferdinand Chacha kutoka mkoani Mwanza (line 1) na upande wa pili ni Soud Lila wa Dar es Salaam (line 2) na mwamuzi wa akiba mezani ni Frank Komba wa Dar es Salaam pia. Kamishina wa mchezo huo ni Juma Mgunda kutoka mkoani Tanga.
Fainali za Kombe la Shirikisho zinakuja baada ya mchuano ulioshindanisha timu 64 za Ligi Kuu Tanzania Bara - VPL (16); Ligi Daraja la Kwanza -FDL (24), Ligi Daraja la Pili – SDL (24).
No comments:
Post a Comment