BEKI wa Mtibwa Sugar, Andrew Vincent 'Dante' amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na Yanga SC jamatatu wiki hii.
Vincent, mmoja wa mabeki wa kati waliofanya vizuri msimu huu
Dante sasa anakwenda kupambana kugombea namba dhidi ya mabeki wengine wa kati wa Yanga, Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro', Kevin Yondan, Pato Ngonyani na Mtogo Vincent Bossou.
Dante sasa anakwenda kupambana kugombea namba dhidi ya mabeki wengine wa kati wa Yanga, Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro', Kevin Yondan, Pato Ngonyani na Mtogo Vincent Bossou.
BEKI huyo wa Kati wa Mtibwa Sugar, amemaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na alisema kuwa timu yoyote inayomhitaji iweke mezani shilingi milioni 50 ili ajiunge nayo. Dante mwenye rasta ameenda mbali kwa kusema hachagui timu ya kuchezea msimu ujao iwe Mtibwa, Simba au Yanga isipokuwa yoyote itakayompa fedha anazotaka tu.
Dante amesaini muda mfupi baada ya kusaini kipa wa Prisons, Beno Kakolanya leo.
Kakolanya pia amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na wafalme hao wa soka ya Tanzania, Yanga SC, jambo ambalo ni pigo kwa mahasimu, Simba SC waliokuwa wanamtaka kipa huyo.
Kakolanya anakwenda kuungana na makipa watatu waliopo Yanga, Deo Munishi ‘Dida’, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Benedicto Tinocco kufanya idadi ya makipa wanne.
Hata hivyo, mustakabali wa Tinocco haueleweki sasa baada ya kusajiliwa kwa Kakolanya mwenye umri wa miaka 22.

MWISHO:
No comments:
Post a Comment