
Simba imefanikiwa kumsajili kiungo wa Mtibwa Sugar, Muzamil Yassin kwa Mkataba wa miaka miwili na sasa inahaha kukamilisha usajili wa kiungo mwingine wa timu hiyo ya Morogoro, Shizza Kichuya.
Muzamil anakuwa mchezaji wa tatu kusaini Simba, baada ya beki Emmanuel Semwanza na kiungo Jamal Mnyate wote kutoka Mwadui ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amekataa kutaja wachezaji waliosajiliwa hadi sasa, kwa madai kuwa watatangaza rasmi kesho, ingawa fununu zilizpo zinabainisha kuwa wachezaji Semwanza, Mnyate na Muzamil ndiyo wamesaini kati ya sita wanaowataka.
Wengine ambao Simba ilikuwa inahaha kukamilisha usajili wao jana ni winga machachari wa Mtibwa Sugar, Shizza Ramadhani Kichuya, Salim Kimenya na Jeremiah Juma wa Prisons.
Huku taarifa kamili ya usajili wa timu hiyo ikitajwa kutolewa kesho.
MWSIHO:
No comments:
Post a Comment