Monday, June 27, 2016

PICHA ZA BOMOABOMOA KATIKA NYUMBA ZA NHC ZILIZOPO MTAA WA KINGO KATA YA SABASABA MKOANI MOROGORO




 Baadhi ya wapangaji wakichukua Frem za Milango

 Wapangaji hao wakiwa na mabati na mbao walizochukua kwenye nyumba hizo
 Meneja wa ukusanyaji Madeni wa shirika la Nyumba la Taifa NHC Mkoa wa Morogoro Japhet Mwanasenga akihojiwa na Waandishi wa habari










Tukio hilo la bomoa bomoa limetokea siku  chache zilizopita katika mtaa wa  Kingo Kata ya Saba Saba Mkoani Morogoro ambapo jumla ya wakazi 22 waliokuwa wanakaa katika nyumba za NHC zilipo mkoani humo walibomolewa nyumba zao. 

Wakazi hao walipewa notisi ya kuhama katika nyumba hizo na shirika hilo la nyumba, lakini ilishindikana baada ya wakazi kwenda kufungua kesi mahakamani.

Akizungumza na Mtandao huu kwa Uchungu huku akitazama Nyumba aliyokuwa ikiishi  ikivunjwa Salima Mrisho alisema yeye na wapangaji wenzake waliishi kwenye Nyumba hizo kwa miaka mingi huku wakiahidiwa kuuziwa Nyumba hizo kama walivyouziwa wafanyakazi wengine wa Serikali . 
Kwa Upande wake msimamizi wa bomoa bomoa hiyo Japhet Mwanasenga ambaye ni Meneja wa Ukusanyaji Madeni ‘NHC’Mkoa wa Morogoro alisema
"Tuliwapa Notisi wakagoma wakaenda Mahakamani tukawashinda, wakakata rufaa pia tukawashinda, kwa kuthamini uwepo wao kwenye nyumbani hizi kwa muda mrefu shirika limeamua kuwapa laki tano kila mmoja kama kiinua Mgongo na kuwaruhusu wachukue mabati,Milango na Matofari”alisema Bw Mwanasenga.

MWISHO:

No comments:

Post a Comment