Sunday, June 26, 2016

TP MAZEMBE KUWASILI LEO SAA TATU USIKU, TAYARI KWA MCHEZO WA JUMANNE DHIDI YA YANGA.


Tokeo la picha la tp mazembe

Mabingwa mara tano Afrika, TP Mazembe ya DRC wanatarajiwa kutua usiku wa leo tayari kwa mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji wao Yanga SC, mchezo utakaochezwa Jumanne katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


TP Mazembe inakuja na kikosi cha wachezaji 18, akiwemo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu.


Kikosi kamili kinachokuja na TP Mazembe ni; Robert Kidiaba, Sylvain Gbohou, Issama Mpeko, Joel Kimwaki, Thomas Ulimwengu, Christian Koume, Jean Kasusula, Salif Coullbaly, Merveille Bope, Jose Badibake, Kissi Boateng na Roger Assale.


Wengine ni Rainford Kalaba, Deo Kanda, Adama Traore, Chriastian Luyindama, Nathan Sinkala na Joas Sakuwaha.

Maofisa wa benchi la Ufundi wanaokuja ni Theobald Binamungu, Mohamed Kamwanya,Dony Kabongo, Frederic Kitengie na Andre Ntime.
Madaktari ni Hurbert Velud, Pamphile Mihayo, Mhudumu Richard Mubemb na Maofisa wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Heritier Yinduka, Arther Kikuni na Meshack Kayembe.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuwasili saa 3:00 usiku na kesho jioni watakafanya mazoezi mepesi katika  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam .
Viingilio katika mchezo huo wa pili kwa kila timu baada ya Mazembe kushinda 3-1 katika mchezo wa kwanza nyumbani dhidi ya Medeama ya Ghana na Yanga kufungwa 1-0 ugenini na MO Bejaia ya Algeria Jumapili iliyopita ni Sh. 7000 kwa majukwaa ya mzunguko na Sh. 30,000 kwa VIP na tiketi zitaanza kuuzwa kesho.

Waamuzi wa mchezo huo ni Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe O'michael wa Eritrea.

MWISHO:

No comments:

Post a Comment