Kiwanda cha nguo
cha 21 Century kilichopo Kihonda Maghorofani mkoani Morogoro Kimeteketea na
moto asubuhi ya leo ya uliosababishwa na hitilafu ya umeme ambapo wafanyakazi
waliokuwa zamu wanasema umeme huo umeanzia katika mashine namba moja na
kusambaa katika nguo na Pamba.
Kiwanda hicho
chenye wafanyakazi zaidi ya 1600 kililazimika kusitisha shughuli zake za
uzalishaji kwa kuwaruhusu wafanyakazi wake kurudi majumbani kupumzika huku
taasisi husika zikiendelea na jukumu la kuzima moto kwa kusaidiana na kikundi
maalumu kilicho kiwandani hapo.
Katika Ajali hiyo askari mmoja wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji amedondokewa na kitu chenye incha kali kichwani wakati akiwa katika harakato za uokoaji na kukimbizwa hospitali ya rufua ya mkoa kwa ajili ya matibabu zaidi.
Akizungumza na
Mtandao huu Meneja uzalishaji wa kiwanda hicho Clement Munisi amesema idadi
kubwa ya mashine ndizo zilizoteketea katika ajali hiyo ya moto huku moto huo
ukianzia katika plate mashine baada ya kuanza kutokea cheche zilizopelekea moto
huo kutokea na kuanza kusambaa sehemu mbalimbali za kiwanda hicho.
Mpaka mtandao
huu unatoka eneo la tukio harakati za kuendelea kuuzima moto huo ulikuwa bado unaendelea
kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho pamoja na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Marobota ya
nguo pamoja na Pamba ndizo zilizoteketea zaidi katika ajali hiyo ya moto, huku
thamani ya vifaa vyote vilivyoteketea na moto huo bado havijabainishwa.
Hata hivyo
wafanyakazi wa kiwanda hicho wameuambia mtandao huu kuwa mashine hiyo namba
moja ambayo ndiyo chanzo cha moto huo imekuwa ikitoa cheche mara kwa mara wakati
wa uzalishaji.
MWISHO:
No comments:
Post a Comment