Wednesday, July 6, 2016

TIMU YA SIMBA KUTUA MOROGORO IJUMAA KUWEKA KAMBI YA MWEZI MMOJA


SIMBA SC inatarajiwa kuondoka mjini Dar es Salaam kesho kutwa kuja Morogoro kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambayo inatarajiwa kuanza kuanzia Agosti 20, mwaka huu.


Na baada ya maandalizi mazuri ya takriban mwezi mzima, Simba imeialika klabu bingwa ya Kenya, Gor Mahia kwa ajili ya kuja nchini kucheza mechi ya kirafiki katika Tamasha la Simba Day, Agosti 8.


Akizungumza na mtandao huu Rais wa Simba, Evans Elieza Aveva alisema kwamba uongozi wa timu hiyo uliamua kuahirisha programu ya mazoezi iliyopangwa kuanza jana mjini Dar es Salaam kwa ajili ya kupisha sherehe za Sikukuu ya Eid El Fitri.


Meneja huyo wa zamani wa Embassy Hotel, Aveva alisema kuwa wachezaji wote waliosajiliwa na timu hiyo watakwenda kambini Morogoro kwa ajili ya kuanza kujifua wakiwa chini ya Kocha Mkuu mpya Mcameroon Joseph Marius Omog ambaye aliwasili nchini wiki iliyopita na kurithi mikoba ya Muingereza Dylan Kerr, aliyefukuzwa Januari.

MWISHO:

No comments:

Post a Comment