Na,Mohamed Ferooz
IFARAKARA/MOROGORO
Ukosefu wa gari la
wagonjwa, uhaba wa watumishi na vifaa tiba ni changamoto ambazo zimeendelea
kuiandama hospital ya Wilaya ya kilombero mkoani Morogoro, hatua iliyopelekea
kushindwa kutoa huduma stahiki kwa wananchi wanaoishi wilayani humo.
Kutokana na ongezeko la
kasi la idadi ya watu Wilayani humo, imeleezwa kuna kila haja kuboresha huduma hizo mhuhimu, ili kukidhi
mahitaji ya huduma za kimatibabu, zinazohitajika wilayani humo.
Akizungumza na mtandao huu wakati akipokea msaada wa magodoro kutoka kwa mbunge mstaafu wa jimbo hilo Abdul Mteketa, Mganga mkuu wa kituo hicho cha Kibaoni Peter Mlenge amesema kutokana na hospitali hiyo kutarajiwa kuwa hospitali ya halmashauri ya mji wa ifakara inabidi wadau na serikali kuongeza jitihada za kuiborsha hospitali hiyo ambayo hali yake sio nzuri kimuonekano pamoja na huduma kutokana na ukosefu wa wataalamu na pamoja na vifaa. .
![]() |
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kilombero Abdul Mteketa akizungumza na waandishi wa Habari ambao hawako kichwani. |
Aliyewahi kuwa mbunge katika jimbo hilo la Kilombero
kupitia chama cha mapinduzi CCM abdul Mteketa anahitikia wito huo na kumua
kutoa msaada wa magodoro 50 katika hospitali hiyo huku magodoro mengine 150 akitoa kwa
watu kwa wazee, wakimama na watu wasiojiweza wilayni humo..
MWISHO:
No comments:
Post a Comment