NA, Happynes James
Morogoro
Katibu wa chama cha
mpira wa miguu manispaa ya Morogoro (MMFA ) Kafale Maharagande amefikishwa mahakamani na taasisi
ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru mkoani humo kwa tuhuma za kutoa
rushwa ya chakula chenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000) kwa wajumbe wa chama hicho hili wamchague
wakati wa uchaguzi.
![]() |
Katibu wa MMFA Kafale Maharagande akiwa Mahakamani |
Akisomewa mashtaka hayo
na mwendesha mashtaka wa Tukukuru mkoani Morogoro Cleonce Cleophace mbele ya hakimu
mkazi Ivan Msacky, mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kutenda kosa hilo julai 24 mwaka
huu wakati wa uchaguzi wa chama hicho ambapo alichaguliwa tena kuwa katibu wa
chama hicho cha mpira wa miguu..
![]() |
Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU mkoani Morogoro Cleonce Cleophace akinena jambo na mmiliki wa Blog Hii. |
Ikiwa umepita
mwezi mmoja na siku moja tangu kufanyika
kwa uchaguzi wa MMFA, ambao ulimtangaza Kafare Maharagande kuwa katibu mkuu wa
chama hicho, mpinzani wake Jofrey Mwatesa hakuridhishwa na matokeo hayo, hatua
iliyopelekea kuandika barua ya kukata rufaa kwa kamati ya uchaguzi na nakala
kupeleka TAKUKURU kupinga matokea hayo kwa madai ya katibu huyo kutoa rushwa ya
chakula kwa wajumbe wa chama hicho.
Kukiwa na hali ya bado
sintofahamu kwa kamati ya uchaguzi iliyosimamia uchaguzi huo kuhusu sakata
hilo, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani humo, wanamfikisha katibu
huyo mahakamani tayari kujibu tuhuma
hizo zinazomkabili.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo amekana kutenda makosa hayo licha ya upande wa TAKUKURU kuikikishia
mahakama kuwa ushahidi wa tuhuma hizo ushakamilika.
Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea tena Septemba mosi mwaka huu huku mtuhimiwa huyo akiwa nje
kwa dhamana.
MWISHO:
No comments:
Post a Comment