Friday, February 21, 2014

WAFANYAKAZI WA MAJI WAASWA KUFANYA KAZI KWA UFANISI


Katika kuelekea kwenye nusu ya pili ya utekelezaji wa matokeo makubwa sasa,Wizara ya maji imewataka watendaji wa idara mbalimbali katika wizara hiyo kufanya kazi kwa ufanisi ili kuhakikisha wizara inafikia malengo ya kiutendaji kwa wakati muafaka.


Akifungua warsha ya mafunzo ya ufanisi kazi kwa watendaji wa idara mbalimbali kutoka wizara ya maji,katibu mkuu wa wizara hiyo Bashiri Mrindoko amesema mafunzo hayo pia yatasaidia katika kutambua maeneo yatakayopewa kipaumbele katika bajeti ijayo.

 Tatizo la ukosefu wa maji nchini hasa katika maeneo ya vijijini limekuwa kero kubwa kwa kipindi kirefu,hali inayopelekea baadhi ya wananchi kupata madhara kutokana na kutumia maji yasiyokidhi vigezo. Ili kukabiliana na tatizo hilo Wizara ya maji imeandaa mafunzo maalumu kwa watendaji wa idara mbalimbali kutoka katika wizara hiyo na kuwataka kuwa wafanisi katika utendaji wa kazi ili wananchi wanufaike na huduma hiyo.


No comments:

Post a Comment