Polisi mkoani morogoro inamshikilia Karume Kauzu Habibu Mkazi wa Riti kwa kujifanya daktari katika
haspitali ya rufaa ya mkoa wa morogoro ambapo amekuwa akioneka maeneo
hayo huku akiwa mevalia mavazi ya udaktari.
Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa jeshi la Polisi Renard Paulo amethibitishwa
kutokea kwa tukio hilo na amesema mtuhumiwa huyo baada ya kukaguliwa
amekutwa na vitambulisho vinne tofauti huku kingine kikionyesha anajiandaa
kurudia mtihani wa kidato cha nne, makazi yake yakiti RITI mkoani Morogoro na
huku kitambulisho chake kimoja kinaonyesha kuwa alikuwa anasoma Kigoma.
![]() |
| Daktari feki aliyevaa koti jeupe Karume Kauzu Habibu akiwa chini ya ulinzi |
Kwa upande wake Daktari bingwa wa upasuaji Francis Semwene
amesema alipata taarifa toka kwa muuguzi wa zamu na kuweka mtego ulifanikisha
kukamatwa kwa daktari huyo feki.
Matukio kama haya yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara nchini
kwa baadhi ya watu wasio waaminifu kujiingizia vipato kwa njia zisizo halali na
kutishia usalama na afya za wananchi.
![]() | |
| Baadhi ya Wauguzi wa afya na wagonjwa wakipigwa na butwaa |





No comments:
Post a Comment