Monday, July 14, 2014

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI WALIA NA KANUNI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA......


Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya siasa

Viongozi wa vyama vya siasa nchini wameiomba serikali kupitia upya sheria na kanuni za uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu.

Hayo yamebainishwa mkoani morogoro na mwenyekiti wa CUF  Prof Ibrahimu Lipumba na Naibu katibu wa Chadema John Mnyika katika mkutano wa  viongozi wa vyama vya siasa ngazi ya taifa ya kujadili maoni ya wadau mbalimbali ya kuboresha  kanuni za uchaguzi wa viongozi wa mamlaka za serikali za mitaa huku wakisema kanuni hizo bado haziko sahihi kwani hazikufanyiwa mabadiliko tangu mwaka 2009. 
Mwenyekiti wa  Chama cha CUF, Pro Ibrahim Lipumba
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, pia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeresi

Viongozi hao pia wamesema serikali hakuzingatia maoni ya wadau kuhusu maboresho ya kanuni  za uchaguzi wa mamlaka za serikali za mitaa tangu mwaka 2009 mpaka sasa, hali inayosababisha uchaguzi huo kuwa sio wa haki.

Kwa upande wake waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu, amesema kuwa baadhi ya mapendekezo katika uchaguzi wa seriakali za mitaa wa 2009 yamefanyiwa kazi Kazi na kweka katika kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa, huku akiwaasa viongozi wa vyama vya siasa kuangalia jinsi ya kuweza kukabiliana na changamoto zilizojitokeza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka  2009
 
Waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu, Hawa Ghasia
Pia amewatoa hofu viongozi wa vyama vya siasa kuhusu kuwa na imani na wakurugenzi  wa  halmashauri wa manispaa zote nchini, kwani wanateuliwa kutokana na uwezo waol binafsi bila kujali itikadi zao za vyama.



Mkutano huo wa viongozi wa vyama vya siasa ngazi ya taifa  utadumu kwa muda siku mbili mkoani Mkoani Morogoro  ukiwa na malengo ya kuboresha kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa  wa mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment