Sunday, May 22, 2016

TAMISEMI YAAGIZA UONGOZI WA MKOA WA MOROGORO KUUNDA KAMATI YA KUCHUNGUZA TUHUMA MATUMIZI MABAYAYA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO ZINAZOMKABILI MKURUGENZI WA GAIRO



Tokeo la picha la Mkuu wa Mkoa wa Morogoro


Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeigiza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuunda kamati ya Uchunguzi ambayo itajihusisha kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo ambazo zimeelekezwa kwa mkurungezi wa Halmashauri ya Gairo  mkoani humo Kibwana Magota.



Imeelezwa kuwa tume hiyo itafanya kazi hiyo ndani ya siku saba na itamuhoji mkurungezi huyo, baadhi ya wakuu wa idara pamoja na madiwani, na baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo, taarifa hiyo itafikishikishwa kwa waziri wa TAMISEMI   kwa ajili ya  kuchukua maamuzi.

Katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha Mei 7 mwaka huu, kiliadhimia kutokuwa na imani na mkurungezi wa Halmashauri hiyo, huku katika kikao cha kamati ya fedha cha Mei 13, wajumbe wa kamati hiyo,  nao , walisusia kikao hicho mpaka hapo tuhuma zinazoelekezwa kwa mkurungezi huyo zitakapofanyiwa kazi.

Hatimaye Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa imeweza kuingilia kati mvutano huo, baada ya kuitaka Serikali ya mkoa kuunda kamati ya uchunguzi, kwa wale ambao tuhuma hizo zinaelekezwa kwao, na taarifa  hizo zifikishwe kwa waziri ndani ya siku ya saba tayari kwa kuwachukulia hatua hayo yamebainishwa na katibu tawala wa mkoa wa morogoro Dr John Ndunguru pamoja na mkuu wa mkoa huo Dr Kebwe Stephen.

Huku mkuu wa Mkoa  wa Morogoro Dr Stephen Kebwe akiwataka  madiwani hao, kukubali kushiriki katika vikao vitakavyoandaliwa na Halmshauri hiyo, wakati suala lao la tuhuma kwa mkuruigenzi wa halmashauri hiyo likifanyiwa.

Madiwani wa Halmashauri ya Gairo waliadhimia kutofanya kazi na mkurungezi wa halamshauri hiyo  kwa madai ya kutoridhishwa na utendaji wake hasa katika kupanga na kufatilia miradi ya maendeleo na kutaka madai yao kufikishwa TAMISEMI.

MWISHO:

No comments:

Post a Comment