Tuesday, May 24, 2016

YANGA KUNDI MOJA NA TP MAZEMBE, PIA YAPEWA MWARABU MMOJA..



Draw ya kupanga makundi mawili ya timu zitakazochuana kuwania kufuzu hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho Afrika imekamilika na kila timu imeshajua itachuana na klabu gani katika hatua hiyo ya nane bora. 


Mabingwa wa Tanzania bara klabu ya Yanga imepangwa Kundi A ambapo itachuana na TP Mazembe (Congo DR), MO Bejaia (Ageria) na Medeama (Ghana). 

Mo Bejaia ni timu pekee kutoka Kaskazini mwa Afrika huku timu tatu zikitoka katika maeneo mengine tofauti ya bara la Afrika. 

Group B lina klabu za Kawkab Athletic, Futh Union Sports (Morocco), Etoile du Sahel (Tunisia) pamoja na Ahly Tripoli (Libya).


Kundi B linazikutanisha timu zote zinazotoka ukanda wa Kaskazini mwa Afrika (timu kutoka mataifa ya Kiarabu) na hiyo imetokana na timu tano za ukanda huo kufuzu hatua nane bora kati ya nane.

MWISHO:

No comments:

Post a Comment