![]() |
| Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Ulrich Matei akiwa na Daktari feki |
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Zakaria Benjamini mkazi wa Tungi Manispaa ya Morogoro baada ya kuingia hospitali ya rufaa kwa nia ya kufanya utapeli na kutaka kutoa huduma kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi Polisi Mkoani humo Ulrich Matei amesema mtuhumiwa huyo ana miaka
35 mkazi wa Tungi manispaa ya Morogoro, na anatuhumiwea kuingia katika hospitali
ya Rufaa mkoani humo kinyume na utaratibu na kujifanya ni Daktari mgeni
anaye kagua huduma zitolewazo katika hospitali hiyo.
Kamanda Matei, amesema mtuhumiwa huyo alifika
hospitalini hapo na kuchukua vazi la kidaktari na kisha kutembelea wodi
mbalimbali akiwahoji wagonjwa juu ya matibabu wanayopatiwa, ambapo muuguzi wa
zamu alimtilia mashaka na kutoa taarifa ndipo jeshi la polisi lilipofanikiwa kumkamata.
kwa upande wao wauuguzi walikuwepo zamu Expiransa Mtama muuguzi wa ICU na Ester Uwizo Muuguzi msaidizi wa zamu wanasema walimbaini daktari huyo kuwa ni feki kutokana na maswali yake aliyokuwa anawauliza wagonjwa alipokuwa anatembelea katika wodi hizo, hatua iliyopelekea wao kutoa taarifa Polisi.
Mtuhumiwa huyo anaendelea
kuhojiwa na jeshi la polisi mkoani humo, na mara baada ya uchunguzi kukamilika
atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabili.
MWISHO:

No comments:
Post a Comment