Kutokana na maombi ya vilabu vingi vya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutaka kuandaa wachezaji kwa ajili ya msimu mpya wa ligi unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi August 20 mwaka huu, Kocha Mkuu wa Tanzania, Charles Boniface Mkwasa ameahirisha kambi iliyokuwa ianze Jumatatu Agosti mosi, mwaka huu.
Wachezaji ambao Mkwasa amewaita wanatoka kwenye vilabu mbalimbali, na ambazo zinaongoza kutoa nyota wengi ni Simba SC, Young Africans SC, Azam FC na Mtibwa Sugar FC ambapo kwa sasa watabaki na vilabu vyao.
Hivyo basi, Mkwasa sasa atakuwa anafuatilia mwenendo wa nyota 24 aliowaita kwenye michezo mbalimbali ya kirafiki wa klabu hizo zinayofanyika kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara (Pre-season matches) na michezo ya raundi ya kwanza na pili ya Ligi Kuu kabla ya kukiita tena kikosi hicho kwa ajili ya safari ya kwenda Nigeria.
Wachezaji walioitwa ni Makipa; Deogratius Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam) na Benny Kakolanya (Yanga), mabeki; Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Mohamed Husein ‘Tshabalala’ (Simba), Juma Abdul (Yanga) na Erasto Nyoni (Azam).
Viungo: Himid Mao, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Ibrahim Jeba, Mwinyi Kazimoto, Farid Mussa, Juma Mahadhi na Hassan Kabunda.
wakati washambuliaji ni Simon Msuva, Joseph Mahundi, Jamal Mnyate, Ibrahim Ajib, John Bocco na Jeremia Juma.
MWISHO:
No comments:
Post a Comment