NJOMBE
Licha ya naibu waziri wa Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi Dkt John Elias Kwandikwa kutoa agizo la kusitisha ujenzi wa jengo refu la Ghorofa Mbele ya uwanja wa Ndege wa mkoa wa Njombe ili kuacha wazi eneo hilo la ndege kupaa, agizo hilo limeonekana kupuziwa kwani ujenzi huo umeendelea kama kawaida.
Agizo la kusitisha ujenzi huo lilitolewa wiki moja iliyopita na naibu waziri huyo wakati akiwa katika ziara mkoani humo kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo barabara , majengo na viwanja vya ndege baada ya kubaini ujenzi huo ambao umetajwa kuweka mazingira ya hatari kwa ndege kupaa endepo kutatokea shida katika kupaa.
Pamoja na Kusitisha ujenzi huo Naibu waziri huyo alifika katika eneo linalotekelezwa mradi huo na kubaini kuwa ujenzi umekuwa ukiendelea bila ya uwepo wa wataalamu hali ambayo inaweza kujakuwa na madhara hapo baadae endapo litajengwa chini ya kiwango na kuagiza wataalamu wote wa ujenzi huo kukaguliwa vyeti vyao.
Blog hii imefika katika eneo la ujenzi na kushuhudia ujenzi ukiendelea na kuzungumza na mkandarasi Enjinia Yusuph Bikube anaetekeleza ujenzi wa jengo hilo la ghorofa ambaye anasema mamlaka za mkoa wa Njombe ikiwemo ya viwanja vya ndege na halmashari zimeafikiana na kuamua kumruhusu mteja wake kuendelea na ujenzi huku zikimtaka kupunguza urefu wa jengo hilo kutoka ghorofa nne hadi mbili.
Siku chache zilzopita akizungumzia Ujenzi wa jengo hilo Dkt kwandikwa alisema ujenzi unapaswa kusimama mara moja huku akimuagiza meneja wa meneja wa uwanja huo Hana Kibopile kufatilia nyaraka za kuruhusiwa kujenga kwani jengo refu kuwepo uwanja wa Ndege ni hatari .
Akizungumza na Blog hii Mmiliki wa jengo hilo Sebastian Sanga amesema ana vibali vyote halali ambavyo vinamruhusu kuendelea na ujenzi huo na kwamba mara tu baada ya naibu waziri kusitisha ujenzi maafikiano yalifanyika ya kupunguza urefu wa jengo hilo lililokuwa lijengwe ghorofa nne na badala yake ziwe mbili na kukili kupata hasara ya zaidi ya shilingi mil 50 na serikali kwani vifaa vingi vimeharibika baada kusitisha ujenzi kwa takriban mwaka.
MWISHO




No comments:
Post a Comment