Monday, February 26, 2018

Tuesday, January 16, 2018

FEDHA BANDIA ZENYE THAMANI YA SHILINGI MIL 40.6 ZAKAMATWA MKOANI MOROGORO

Morogoro
Na, OmaryHussein

Watu watano wanashikiliwa na Polisi mkoani Morogoro, kwa makosa tofauti yakiwemo ya watu  wawili kukutwa na pesa bandia zenye thamani ya zaidi ya shilingi  Milion 40.6 na mabunda 22 ya karatasi zinazotumika  kutengeneza  noti hizo, huku wengine wawili wakikutwa na vipande 4 vya pembe za Ndovu.


Monday, January 15, 2018

WATU 11 WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE SITA KUJERUHIWA BAADA YA GARI AINA YA HIECE KUGONGANA NA MALORI MATATU

KAGERA, 
Na, Mariam Emily
Watu 11 wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kutokana na ajali ya gari aina ya hiece kugongana na malori matatu katika kijiji cha Mubigera kata ya Nyantakara wilaya ya biharamulo mkoani kagera wakati wakisafiri kutoka wilaya ya kibondo kuelekea kahama mkoani Shinyanga.
Image may contain: one or more people and outdoor

Sunday, January 14, 2018

BOMOA BOMOA MWANZA YAWALIZA WAFANYABIASHARA WA SAMAKI NA DAGAA


Kampuni hodhi ya rasilimali za reli nchini (Rahco) imeanza utekelezaji wa kubomoa nyumba zote zilizojengwa ndani ya njia ya reli katika mkoa wa Mwanza huku zaidi ya wafanyabiashara 200 wa samaki na dagaa jijini humo wakikosa sehemu ya kwenda kufanyia biashara zao baada ya kubomolewa vibanda vyao.

Thursday, December 28, 2017

MAUTI ILIYOZIKWA ZAIDI YA MWEZI MMOJA ULIOPITA YAFUKULIWA KWA LENGO LA KUCHUNGUZWA

GAIRO,MOROGORO
NA, OMARY HUSSEIN

Huzuni na simanzi zimetawala kwa zaidi ya masaa nne kwa wakazi wa kijiji cha Kilimani kata ya Msingisi wilaya ya Gairo mkoani Morogoro baada ya familia ya watoto wanne wakiongozwa na mama yao mzazi kufika kijijini hapo na kufukua kaburi alipozikwa baba yao aliyezikwa miezi miwili iliyopita, wakidai kuwa na mashaka na kifo chake ikiwa ni sehemu moja wapo ya kutekeleza agizo la mahakama ya hakimu Mkazi mkoa wa  Morogoro.

UJENZI WA GHOROFA UMEKULA KERO KWA UWANJA WA NDEGE WA NJOMBE

NJOMBE
Licha ya naibu waziri wa Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi Dkt John Elias Kwandikwa kutoa agizo la kusitisha ujenzi wa jengo refu la Ghorofa Mbele ya uwanja wa Ndege  wa mkoa wa Njombe ili kuacha wazi eneo hilo la ndege kupaa, agizo hilo limeonekana kupuziwa kwani ujenzi huo umeendelea kama kawaida.