Sunday, May 22, 2016

AFRICAN SPORT, MGAMBO JKT NA COASTAL UNION WASHUKA DARAJA VPL 2015/2016




Kivumbi cha ligi kuu Tanzania bara kimefika tamati leo katika viwanja 8 tofauti nchini huku ikishuhudiwa tena timu mbili zikijiunga na timu ya coastal Union tayari kushuka daraja  ambazo ni timu zote kutoka mkoani Tanga yaani Coastal Union, Mgambo JKT, na African Sports. TANGA kunaniiiiii!!!!



Katika michezo hiyo, timu ya Simba Sport ikicheza katika uwanja wa nyumbani (Uwanja wa Taifa)  imepoteza mchezo wake dhidi ya JKT Ruvu baada ya kukubali kupigo cha Goli mbili kwa moja, huku magoli ya JKT RUVU yakifungwa na Abdulhaman Mussa katika dakika ya 2 na 30 huku goli la kufutia machozi la simba likifungwa na Mussa Mgosi.

Katika uwanja wa Manungu Mkoani Morogoro, wakata miwa wa Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa Goli 2 kwa sifuri dhidi ya wana kimanumanu African Sport ya mkoani Tanga. Magoli hayo ya wazee wa sukari yamewekwa kimiani na Hussein Javu dk ya 1 na goli la pili limewekwa kimiani na Jafary Kibaya dk ya 82 ya mchezo huo, mpaka filimbi ya mwisho Mtibwa Sugar 2 – African Sport 0 hatua inayopelekea timu hiyo kushuka daraja kuongana na ndugu zao.

Katika uwanja wa chamanzi, Mbagala  wana ramba ramba wa Azam FC wameradhimishwa sare ya kufungana goli moja kwa moja  na JKT Mgambo ya Kibuku Mkoani Tanga, goli la Azam FC limefunga na Ramadhani Singano huku la mgombo likifungwa kwa njia ya Penalt, hatua iliyopekea timu hiyo pia kujiunga na coastal, Africani Sport kushuka daraja.

Katika uwanja wa Majimaji Mkoani Songea, mabingwa  wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga wamelazimishwa sare ya kufungana magoli mawili kwa mawili na timu ya Majamaji FC ya mkoani humo.

Katika uwanja wa CCM kirumba mkoani mwanza , wenyeji Toto African wamekubali kichapo cha goli moja kwa sifuri kutoka kwa timu ya Stand United ya mkoani Shinyanga.

Mkoani Mbeya timu ya Tanzania Prisons  imetoa kipigo kwa timu ya  Coastal Union baada ya kuifunga goli mbli kwa sifuri na kushika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.

Mkoani Shinyanga timu ya kagera sugar imeibuka na ushindi wa goli mbili kwa sifuri dhidi ya timu ya Mwadui FC.

Kwa matokeo hayo ya leo timu ya AZAM FC inashika   nafasi ya pili ya msimo wa ligi kuu Tanzania bara, huku SIMBA SPORT KLABU ikishika nafasi ya Tatu na Timu ya Tanzania Prison ikishika nafasi ya nne nay a tano inashikwa na wazee wa  sukari Mtibwa Sugar.

Kwa upande mwingine matokeo hayo yamesababisha timu mbili kujiunga na timu ya Coastal Union kushuka daraja baada ya kupoteza michezo yao, timu hizo ni Mgambo JKT na African Sport.
KIKOSI CHA JKT MGAMBO
Huku mchezaji  Amiss Tambwe wa YANGA akiibuka  mfungaji bora wa mwaka 2015/2016.

Historia inaonyesha haikuwahi kutokeanchini  timu tatu zinazotoka sehemu moja kushuka daraja, hatua inayopelekea wadau wa soka kujiuliza TANGA kunaniii!!!!!!!!!

MWSIHO:


No comments:

Post a Comment