Chama cha soka Manispaa ya Morogoro MMFA kimemsimamisha kazi mjumbe wake Alex Bulengwa kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha shilingi laki mbili za makusanyo ya mapato ya getini katika uwanja wa sabasaba Mkoani Morogoro.
Hatua ya kusimishwa kwake amekuja baada ya chama hicho kuwa katika maandalizi ya uchaguzi wa uongozi mpya wa chama hicho, huku katibu wa chama hicho Kafale Maharagande akisema suala la kusimamishwa kwake linapelekwa kwenye mkutano mkuu utakaofanyika tarehe 15 mwezi huu kwa lengo la kumjadili mjumbe huyo.
![]() |
KATIBU WA CHAMA CHA SOKA MANISPAA YA MOROGORO, KAFALE MAHARAGANDE. |
Hatua hii inakuja ikiwa ni muendelezo wa sera ya raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ya kutumbua majipu, ambapo katika sekta ya michezo viongozi waliopewa nafasi hiyo na wadau wa michezo wanatumia sera hiyo kuweza kutumbua vijipu uchungu ambavyo vimekuwa vikikiuka sheria na kanuni za mchezo wa mpira wa miguu.
Mjumbe huyo anadaiwa kutumia fedha za kiingilio za mashabiki katika uwanja wa sabasaba kwa ajili ya matumizi yake binafsi shilingi elfu kumi na tano, hatua iliyopelekea chama hicho kumsimamisha kazi huku wakipanga kumjadili katika mkutano mkuu utakaofanyika tarehe 15 mwezi wa tatu mwaka huu.
Kwa upande mwingine katibu Kafale Maharagande ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa soka mkoani hapa kuweza kujitokeza pindi nafasi mbalimbali za uongozi wa chama hicho zitakapotangazwa kwa ajili ya kugombea.
MWISHO:
No comments:
Post a Comment