Waswahili wansema Kipofu kaona mwezi,
baada ya kukaa kwa muda mrefu na kiu ya
ushindi, hatimaye klabu ya simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli moja
kwa sifuri dhidi ya timu ya wakata miwa wa turiani Mtibw sugar.
Mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ulianza kwa kasi huku kila timu
ikishambulia lango la mpinzani wake, mpaka
Dakika 45 za kwanza timu zote zilikwenda mapumziko wakiwa hawajafungana.
Kipindi
cha pili cha mchezo kila timu ilifanya
mabadiliko, mabadilko ambayo yamekuwa na manufaa kwa timu ya Simba, baada ya
dakika 70 kuandika bao safi kupitia kwa
mchezaji wake Abdul Banda baada ya kuunganisha kross safi ya Mohamed Hussein.
Hadi Filimbi ya Mwisho ya Refa ya Alex Mahagi kutoka Mkoani Mwanza Mnyama Simba goli
moja, na wazee wa sukari Mtibwa sugar Sifuri.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo kocha wa timu ya mtibwa sugar Meck Mexime aliweza kuongea na mtandao huu akisema maamuzizi ya marefa yanachangaia kuzididmiza timu ndogo zinazoshiriki ligi kuu Tanzania, huku akitoa ushauri kwa TFF kurekebisha baadhi ya kasoro mbalimbali zilizojitokeza .
Kwa upande mwingine mashabiki wa timu Simba hakuwasita kuonyesha furaha yao huku wakiwa hawaamini kama kweli timu hiyo imeibuka na
ushindi dhidi ya wakata miwa wa Mtibwa Sugar, huku wakisema viongozi ndio chanzo cha kusababisha timu hiyo kufanya vibaya katika michezo yake ya ligi kuu kutokana na kila mmoja kuwa na wachezaji wake anaowamiliki.
Kwa matokeo hayo timu ya Simba imefikisha pointi 62, na kuendelea kushika nafasi ya tatu huku timu ya Mtibwa ikibaki na na pointi zake 47 Kibindoni.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment