Jeshi
la polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kumkamata dereva Seif shabani wenye umri wa miaka 40 mkazi wa Bacho mkoani Tabora Dereva wa Basi
lenye namba za Usajili T 909 BXK
mali ya kampuni ya NBS aliye sababisha ajali iliyo pelekea vifo vya watu
watano na majeruhi 27 june 20 mwaka huu
katika eneo CHAKWALE wilayani Gairo barabara ya Morogoro-Dodoma.
Kaimu
kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP-Leonce Rwegasira amesema dereva huyu
alitoroka mara baada ya kusababisha ajali hiyo ambapo chanzo cha ajali kilikua ni mwendokasi uliomfanya dereva kushindwa kulimudu gari hilo ambalo liliacha njia na kupinduka.
Kamanda
huyo amesema uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika kwa kumuohoji mtuhumiwa na
pale utakapokamilika utafikwishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma
zinazomkabili.
MWISHO:
No comments:
Post a Comment