![]() |
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP-Leonce Rwegasira akionyesha risasi hizo kwa Waandishi wa Habari |
Jeshi
la Polisi Mkoani Morogoro limefanikiwa kukamata
risasi 853 zilizokuwa zikitumika kwenye
silaha aina ya G – 3 zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye dumu na kutelekezwa pembezoni mwa mto wa Ngerengere maeneo ya Kihonda mkoani humo.
Kaimu kamanda wa Polisi Mkoani humo ACP Leonce Rwegasira amesema tukio hilo limetokea Jun 20 mwaka huu katika kata ya Kihonda mkoani humo baada ya askari waliokuwa doria kupewa taarifa na raiawema na ndipo wapokwenda eneo la tukio wakakuta dumu likiwa limewekwa pembezoni wa mto Ngerengere na kukuta limejaa risasi.
Kaimu
wa Kamanda Rwegasira amesema jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi ili kuweza kubaini wamiliki wa risasi hizo ili kuweza kuwachukulia hatua
stahiki za kisheria.
MWISHO:
No comments:
Post a Comment