Monday, October 17, 2016

WAZIRI LUKUVI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA OFISI YA MASJALA YA ARDHI MANISPAA YA MOROGORO

Na, Omary Hussein, Morogoro.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,

Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi ya Masjala ya Ardhi Manispaa ya Morogoro na kukuta hati zaidi ya 100 ambazo zimekamilika lakini bado hazijatolewa kwa wahusika huku Maofisa wa Ardhi katika ofisi hiyo wakishindwa kutoa sababu za msingi za kuchelewesha kutolewa kwa hati hizo.

Kufuatia hali hiyo Waziri lukuvi ametoa mwezi mmoja kwa mkurugenzi wa manispaa ya morogoro pamoja na Afisa Ardhi mteule kuhakiksha hati zote zinatolewa kwa wahusika na endapo itashindikana basi atawachukulia hatua za kinidhamu.
Katika hatua nyingine imebainika kuwa asiilimia 85 ya nyumba katika manispaa ya maorogoro zimejengwa katika makazi yasiyo Rasmi ambapo imetajwa kuwa ni asilimia 15 pekee ndizo zmejengwa katika makazi yanayo tambuliwa kuwa rasmi.
Ziara ya waziri Lukuvi mkoani Morogoro imelenga kuhamasisha zoezi la Urasimishaji wa ardhi ambapo ametoa hati miliki kwa wakazi wa Mtaa wa Bigwa ambao wameshiriki katika urasimishaji wa maeneo yao.
MWISHO:

No comments:

Post a Comment