Manyoni, Singida.
Baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Manyoni limewafukuza kazi watumishi watatu wa halmashauri hiyo kwa makosa tofauti yakiwemo uzembe kazini uliosababisha kifo cha mjamzito mmoja wakati akijifungua.
Akitangaza uamuzi huo, mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mosses Mathonya katika baaraza la madiwani katika mkutano wa kawaida alisema watumishi watatu wamefukuzwa kutokana na tuhuma mbali mbali,zikiwemo uzembe wa madaktari Mika Iloti muuguzi msaidizi daraja la kwanza na mtaalam wa kuchoma dawa za usingizi pamoja na Dk John Amita mtaalam wa upasuaji kuchelewesha upasuaji wa mzazi na kusababisha kifo cha Sai Richard.
Aidha mtumishi mwingine aliyefukuzwa ni Genesius Rugemalira mkuu wa kitengo cha ununuzi halmashauri hiyo anatuhumiwa kwa makosa mawili ambayo ni kupotosha bodi ya Zabuni katika kumpata Mzabuni na kununua mitungi ya gesi 242 kwa mzabuni ambaye hakuidhinishwa na bodi ya zabuni na kusababisha hasara ya Tsh 10,648,000 na katika kosa la pili anatuhumiwa kufanya matendo yaliyo kinyume na maslahi ya umma kinyume na kanini no.42 aya ya 10 sehemu (a) ya jedwali la kwanza la kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2013 na kumsababishia mwajiri hasara.
Katika hatua nyingine baadhi waheshimiwa madiwani wamemtaka mganga mkuu wa hospitali ya halmashauri Nelson Bukuna kutoa ufafanuzi wa kina kuhusiana ukosefu wa baadhi ya dawa alieleza kuwa kukosekana kwa dawa hizo kunatokana kucheleweshwa kwa fedha kutoka wizarani.
Bukuna alisema tatizo la kukosekana kwa baadhi ya dawa limejitokeza hivi karibuni na kwamba awali halikuwepo na kwamba tatizo hili limejitokeza mwezi huu na hivyo kama italetwa tatizo hilo litaisha.
Aidha kwa upande wa mbunge wa Manyoni Daniel Mtuka alisema fedha zipo hivyo utaratibu wa kununua dawa ufanyike."Dawa zipo naomba nishirikishwe,ili niwasiliane na waziri mwenye dhamana na hata Rais alishasema Fedha zipo suala la dawa lisiwe tatizo"alisema Mtuka.
Kwa upande wa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Charles Fussi aliwataka viongozi kuacha siasa na blabla nyingi za kuwadanganya wananchi na kwamba huu siyo wakati wa siasa na badala yake wafanye kazi kwa vitendo."Sasa hivi hakuna hela iliyoletwa kwa ajili ya dawa,serikali kwa mwezi huu haijatoa hela,sikuzungumza tu,watu kwenye kazi hatutaki blabla hela haijaletwa ikiletwa lazima wananchi wajue"alisema Fussi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment