Wednesday, May 18, 2016

YANGA YATINGA HATUA YA MAKUNDI LICHA YA KUFUNGWA GOLI MOJA, CANAVARO ATOLEWA KWA KADI NYEKUNDU.



Pamoja na figisu figisu walizofanyiwa mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Tanznia Bara,Yanga SC wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho la soka Afrika (CAF Confederation Cup) baada ya leo kufungwa goli 1-0 na GD Sagrada Esperanç ya Angola.


Yanga SC wametinga hatua hiyo kwa matokeo ya jumla ya goli 2-1, baada ya kufanikiwa kuwafunga goli 2-0 katika mchezo wa awali uliochezwa siku 10 nyuma jijin Dar es salaam kabla ya kupoteza leo kwa goli 1-0.

Katika mchezo huo GD Sagrada Esperanç waliandika goli lao pekee  katika dakika ya 25 kupitia kwa Kabungula na kupeleka mchezo kumalizika kwa GD Sagrada Esperanç kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Yanga SC walimaliza wakiwa pungufu baada ya Nadir Haroub Cannavaro kupewa kadi nyekundu katika dakika ya 87 kabla ya GD Sagrada Esperanç kuzawadiwa penati katika dakika ya 89 na kipa Deo Munish Dida alipangua penati hiyo.

Yanga inaungana na TP Mazembe katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho ambayo yatapangwa hapo baadae. 

No comments:

Post a Comment