Tuesday, June 7, 2016

YANGA YAMFUNGISHA VIRAGO KIUNGO WAKE WA KIMATAIFA, MBUYU ASAINI MIAKA MIWILI TENA




Kiungo  wa Kimataifa wa Yanga kutoka Niger Issoufou Boubacar Garba akipewa mkono wa kwa heri na timu hiyo ya Jangwani baada ya kupewa  barua ya kuvunjiwa   mkataba wake na timu hiyo, huku beki Mkongomani anayeweza kucheza nafasi za kiungo pia, Mbuyu Junior Twite ameongeza Mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea timu hiyo.


Habari ambazo blog hii imezipata kutoka Yanga SC jioni hii zinasema kwamba Mbuyu amesaini leo saa chache baada ya Garba kupewa barua yake  ya kuachana na timu hiyo.

 Garba ameambiwa tu anaachwa kwa sababu ya kushindwa kuwa katika kiwango kinachohitajika kwa matumizi ya timu, wakati Mbuyu kwa mara nyingine anavuna matunda ya jitihada zake uwanjani.

Garba alisajiliwa Yanga SC Desemba mwaka jana baada ya majaribio ya siku mbili tu, lakini tangu hapo amecheza mechi 11 tu na kufunga mabao matatu likiwemo lile la katika sare ya 1-1 na Al Ahly ya Misri mjini Dar es Salaam katika Ligi ya Mabingwa Afrika miezi miwili iliyopita.


Kabla ya Yanga, Garba amewahi kuchezea AS FAN na AS Douanes  za kwao Niger, Muangthong United na Phuket za Thailand, Club Africain na ES Hammam-Sousse za Tunisia.


Mbuyu Twite aliyesajiliwa Yanga SC miaka minne iliyopita kutoka APR ya Rwanda, katika kipindi chote amecheza mechi 135 na kufunga mabao manne.


MWISHO:

No comments:

Post a Comment