Showing posts with label Paul Wa Pili Blog. Show all posts
Showing posts with label Paul Wa Pili Blog. Show all posts

Tuesday, January 16, 2018

FEDHA BANDIA ZENYE THAMANI YA SHILINGI MIL 40.6 ZAKAMATWA MKOANI MOROGORO

Morogoro
Na, OmaryHussein

Watu watano wanashikiliwa na Polisi mkoani Morogoro, kwa makosa tofauti yakiwemo ya watu  wawili kukutwa na pesa bandia zenye thamani ya zaidi ya shilingi  Milion 40.6 na mabunda 22 ya karatasi zinazotumika  kutengeneza  noti hizo, huku wengine wawili wakikutwa na vipande 4 vya pembe za Ndovu.


Sunday, January 14, 2018

BOMOA BOMOA MWANZA YAWALIZA WAFANYABIASHARA WA SAMAKI NA DAGAA


Kampuni hodhi ya rasilimali za reli nchini (Rahco) imeanza utekelezaji wa kubomoa nyumba zote zilizojengwa ndani ya njia ya reli katika mkoa wa Mwanza huku zaidi ya wafanyabiashara 200 wa samaki na dagaa jijini humo wakikosa sehemu ya kwenda kufanyia biashara zao baada ya kubomolewa vibanda vyao.

Tuesday, December 5, 2017

KESI INAYOWAKABILI WABUNGE WA CHADEMA SUZANA KIWANGA NA PETER LIJUALIKALI YAPIGWA KALENDA MPAKA DESEMBA 6 MWAKA HUU

Na, Omary Hussein, Morogoro


Mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Morogoro, kwa mara nyingine imeshindwa kutoa dhamana kwa Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Peter Lijualikali wa Kilombero pamoja na Suzani Kiwanga wa Mlimba na washtakiwa wengine 34 wa Chama hicho, baada ya kutokea mvutano wa kisheria baina ya upande  wa Mawakili wa Serikali na ule wa utetezi, juu ya kiapo kilichowasilisha na Serikali cha kupinga washtakiwa hao kupatiwa dhamana, hatua iliyopelekea Hakimu Ivan Msaki, kuhairisha tena kesi hiyo hadi Desemba 6, watakapojadili tena kiapo hicho.

Saturday, August 26, 2017

WATUMISHI WATATU WILAYA YA MANYONI WAFUKUZWA KAZI KWA UZEMBE KAZINI

Manyoni, Singida.

Baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Manyoni limewafukuza kazi watumishi watatu wa halmashauri hiyo kwa  makosa tofauti yakiwemo uzembe kazini uliosababisha kifo cha  mjamzito mmoja wakati akijifungua.

Wednesday, January 11, 2017

MBUNGE WA JIMBO LA KILOMBERO AHUKUMIWA MIEZI SITA JELA

Kilombero, Morogoro.


Mahakama ya Wilaya ya Kilombero imemuhukumu kifungo cha miezi Sita mbunge wa Jimbo Kilombero mkoani Morogoro kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Peter Lijualikali wenye miaka (30) mara baada ya kumkuta na hatia ya kufanya fujo na kusababisha taharuki katika uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Machi Mosi mwaka 2016 mwaka wa jana.


Friday, August 19, 2016

VIJANA 9100 KUTOKA MIKOA MITANO WAPATIWA MAFUNZO YA UFUNDI STADI NA VETA KWA LENGO LA KUWAWEZESHA KIUCHUMI

Jumla ya vijana 9100 wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kutoka katika mikoa ya Dar es salaam,Lindi, Morogoro,Mtwara na Pwani,wamepatiwa elimuya ufundi stadi, kwa lengo la kuwakwamua kutoka katika umaskini, huku kipaumbele kikitolewa kwa wenye ulemavu.

MKuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Kebwe Steven  Kebwe akikagua moja  ya bidhaa ya zilitengenezwa na vijana waliopata elimu ya stadi za kazi katika kijiji cha Mchomwe wilayani Kilombero mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Kebwe Steven Kebwe akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mlimba Suzana Kiwanga wakiangalia bidhaaa zilizotengenezwa na vijana waliojiajiri wenyewe mara baada ya kupata elimu ya ufundi stadi kutoka VETA.
Baadhi ya vijana waliyohitimu elimu ya mafunzo ya stadi za kazi kutoka katika kijiji c ha Mchomwe Wilayni Kilombero

Vijana walipata elimu ya udereva kutoka chuo  cha VETA - Mikumi, wakishangilia kwa furaha mara baada ya kupewa Leseni zao za udereva
Vijana Waliopata elimu ya stadi za kazi za ushonaji na Mapambo wakifurahi 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Kebwe Steven Kebwe ( wa Tano toka kulia na Kushoto ) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Jemsi Lionyo  ( wa nne kutoka Kushoto), Mbunge wa Jimbo la Mlimba Suzana Kiwanga ( wa nne Kutoka  Kulia), Mkurugenzi wa Veta kanda ya Mashariki Asanterabi Kanza ( wa tatu kutoka Kulia), Meneja wa Mradi wa Plan International Simon Ndembeka (wa tatu kustoka Kulia), Meneja wa mradi wa Plan International tawi la Ifakara Majani wa pili kutoka kulia na wengineo 
Kipaji chako ndio ajira yako, mmoja kati ya vijana walipewa elimu na VETA akionyesha ustadi wake katika sekta ya umeme


Mafunzo hayo yametolewa na  VETA kwa kushirikiana na  Plan International, yakiwa na mkakati wa kuwawezesha vijana 57,300 wanaoishi katika mazingira magumu hasa maeneo ya vijijini, kupatiwa elimu ya kujiwekea akiba na kuwawezesha kufungua miradi mbalimbali itakayosaidia kuwainua kiuchumi.

Mafunzo hayo ya ufundi stadi yamelenga kuwafikia vijana husika maeneo wanayoishi, kwa mifumo ya nadharia na vitendo na pia kwa njia ya uanagenzi, kwa lengo la kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 vijana wengi na wanaoishi katika mazingira magumu wanasaidiwa ili kujikwamua kiuchumi.

Katika mahafali ya kwanza yalifanyika katika katika kijiji cha mchomwe na ifakara mjini mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr kebwe Steven Kebwe, huku wito ukitolewa kwa mashiriki mengine kuweza kujitokeza na kuwawezesha vijana hasa wale wanaoishi katika mazingira magumu kwa lengo la kuwakwamua,


MWISHO:

Wednesday, July 20, 2016

MIKOA YA DAR ES SALAAM NA DODOMA YAONGOZA KWA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Takwimu zilizotolewa na wizara ya afya, maendeleo ya jamii jinsia , watoto na wazee nchini zinaonyesha kuwa mkoa wa Dar es salaam na Dodoma inaongoza kwa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja

Thursday, July 7, 2016

IDADI YA WATU WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA BASI LA CITY BOY YAONGEZEKA, WAFIKIA 32


Idadi ya watu waliokufa katika ajali iliyohusisha mabasi mawili ya Kampuni ya City Boy imeongezeka na kufikia 32 baada majeruhi aliyekuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) kufariki dunia.

Wednesday, June 29, 2016

HABARI KATIKA PICHA: PICHA MBALIMBALI ZA RAISI MAGUFULI AKIWAAPISHA WAKUU WA MIKOA WAPYA, NA BAADAYE KUONGEA NA MA - DC WAPYA.





MAKAMU WA RAISI AWATAKA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA KUKAMILISHA ZOEZI LA MADAWATI KABLA YA JUNE 30


Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu amewataka wakuu wa wilaya na mikoa kuhakikisha wanamaliza zoezi la upatikanaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari.

Mhe. Suluhu ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wakuu wa wilaya na mikoa walipokuwa Ikulu wakila kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa mikoa yao.

Monday, June 27, 2016

KAMISAA ATAKA MASHABIKI 40,000 TU MCHEZO WA YANGA NA TP MAZEMBE, MASHABIKI WAHIMIZWA KUWAHI MAPEMA UWANJANI



UWANJA wa Taifa, Dar es Salaam una uwezo wa kuchukua watu 60,000, lakini kesho utafungwa wakati wa mchezo wa Yanga na TP Mazembe ya DRC baada ya mashabiki 40,000 kuingia.
Hayo ni maagizo ya Kamisaa wa mchezo huo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, ambao mashabiki wataingia bure, Celestine Ntangungira kutoka Rwanda.


PICHA ZA BOMOABOMOA KATIKA NYUMBA ZA NHC ZILIZOPO MTAA WA KINGO KATA YA SABASABA MKOANI MOROGORO




 Baadhi ya wapangaji wakichukua Frem za Milango

KITWANGA AKABIDHI RASMI OFISI KWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akizungumza na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kushoto) pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano.  

Sunday, June 26, 2016

MKUU WA MKOA WA MARA, MAGESA MALONGO ATENGULIWA KUWA MKUU WA MKOA NAFASI YAKE YACHUKULIWA NA CHARLES MLINGWA, ORODHA YA WAKUU WILAYA WAPYA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

TP MAZEMBE KUWASILI LEO SAA TATU USIKU, TAYARI KWA MCHEZO WA JUMANNE DHIDI YA YANGA.


Tokeo la picha la tp mazembe

Mabingwa mara tano Afrika, TP Mazembe ya DRC wanatarajiwa kutua usiku wa leo tayari kwa mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji wao Yanga SC, mchezo utakaochezwa Jumanne katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

WAZIRI NCHEMBA AWAONYA POLISI WANAOKIUKA MAADILI YA JESHI HILO



WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi Polisi kutotumia nguvu kubwa katika mambo yasiyokuwa na manufaa kwa wananchi ila nguvu hizo zitumike kupambana na biashara ya dawa za kulevya kwa maslahi  ya taifa.

Sunday, June 19, 2016

MOROGORO: WATU WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA KULA MIHOGO INAYOSADIKIWA KUWA NA SUMU

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro  Ulrich Mtei akizungumza na Waandishi wa Habari ambao hawako Pichani


Watu watatu  wamefariki Dunia na wengine wawili kujikuta katika hali mbaya, mara  baada ya kudaiwa kula mihogo  inayodhaniwa kuwa na sumu, katika kijiji cha Kauzeni  kilichopo kata ya Mzinga Manispaa ya Morogoro huku kati yao,  wawili wakiwa ni ndugu wa familia moja.