Friday, August 19, 2016

VIJANA 9100 KUTOKA MIKOA MITANO WAPATIWA MAFUNZO YA UFUNDI STADI NA VETA KWA LENGO LA KUWAWEZESHA KIUCHUMI

Jumla ya vijana 9100 wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kutoka katika mikoa ya Dar es salaam,Lindi, Morogoro,Mtwara na Pwani,wamepatiwa elimuya ufundi stadi, kwa lengo la kuwakwamua kutoka katika umaskini, huku kipaumbele kikitolewa kwa wenye ulemavu.

MKuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Kebwe Steven  Kebwe akikagua moja  ya bidhaa ya zilitengenezwa na vijana waliopata elimu ya stadi za kazi katika kijiji cha Mchomwe wilayani Kilombero mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Kebwe Steven Kebwe akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mlimba Suzana Kiwanga wakiangalia bidhaaa zilizotengenezwa na vijana waliojiajiri wenyewe mara baada ya kupata elimu ya ufundi stadi kutoka VETA.
Baadhi ya vijana waliyohitimu elimu ya mafunzo ya stadi za kazi kutoka katika kijiji c ha Mchomwe Wilayni Kilombero

Vijana walipata elimu ya udereva kutoka chuo  cha VETA - Mikumi, wakishangilia kwa furaha mara baada ya kupewa Leseni zao za udereva
Vijana Waliopata elimu ya stadi za kazi za ushonaji na Mapambo wakifurahi 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Kebwe Steven Kebwe ( wa Tano toka kulia na Kushoto ) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Jemsi Lionyo  ( wa nne kutoka Kushoto), Mbunge wa Jimbo la Mlimba Suzana Kiwanga ( wa nne Kutoka  Kulia), Mkurugenzi wa Veta kanda ya Mashariki Asanterabi Kanza ( wa tatu kutoka Kulia), Meneja wa Mradi wa Plan International Simon Ndembeka (wa tatu kustoka Kulia), Meneja wa mradi wa Plan International tawi la Ifakara Majani wa pili kutoka kulia na wengineo 
Kipaji chako ndio ajira yako, mmoja kati ya vijana walipewa elimu na VETA akionyesha ustadi wake katika sekta ya umeme


Mafunzo hayo yametolewa na  VETA kwa kushirikiana na  Plan International, yakiwa na mkakati wa kuwawezesha vijana 57,300 wanaoishi katika mazingira magumu hasa maeneo ya vijijini, kupatiwa elimu ya kujiwekea akiba na kuwawezesha kufungua miradi mbalimbali itakayosaidia kuwainua kiuchumi.

Mafunzo hayo ya ufundi stadi yamelenga kuwafikia vijana husika maeneo wanayoishi, kwa mifumo ya nadharia na vitendo na pia kwa njia ya uanagenzi, kwa lengo la kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 vijana wengi na wanaoishi katika mazingira magumu wanasaidiwa ili kujikwamua kiuchumi.

Katika mahafali ya kwanza yalifanyika katika katika kijiji cha mchomwe na ifakara mjini mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr kebwe Steven Kebwe, huku wito ukitolewa kwa mashiriki mengine kuweza kujitokeza na kuwawezesha vijana hasa wale wanaoishi katika mazingira magumu kwa lengo la kuwakwamua,


MWISHO:

No comments:

Post a Comment