Morogoro
Na, OmaryHussein
Watu watano wanashikiliwa na Polisi mkoani Morogoro, kwa makosa
tofauti yakiwemo ya watu wawili kukutwa na pesa bandia zenye thamani ya
zaidi ya shilingi Milion 40.6 na mabunda 22 ya karatasi
zinazotumika kutengeneza noti hizo, huku wengine wawili wakikutwa
na vipande 4 vya pembe za Ndovu.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani Morogoro SACP Urlich
Matei, kukamatwa kwa watuhumiwa wote ni juhudi ziliztotokana na taarifa
kutoka kwa raia wema, ambapo wapo waliotoa taarifa za uwepo wa biashara ya
utengenezaji wa fedha bandia katika Mtaa wa Kihonda maeneo ya Yespa, nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro,
na baada ya kufaatilia taarifa hizo, ndipo wakafanikiwa kuwakamata watuhumiwa
hao ambao wamejulikana kwa majina ya Osona Oriko (22yrs) mkazi wa Kihonda
pamoja na Yusufu Abdul (12yrs) mkazi pia wa kihonda .
Aidha askari wa jeshi hilo kwa kushirikiana na maafisa wa
wanyama pori Tarafa ya Mikumi, wamefanikiwa kuwakamata, watu wawili
waliojulikana kwa majina ya Shamte Mohamed (22yrs) na Selemani Meya (23yrs)
wote wakazi wa ludewa wilayani Kilosa wakiwa na vipande vinne vya pembe za
ndovu wakiwa wamevihifadhi katika mfuko wa rambo mweusi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SaCP Matei amesema
watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na watafikishiwa mahakamani baada ya
uchunguzi kukamilika.
MWISHO.


No comments:
Post a Comment