Monday, February 26, 2018

BREAKING NEWS: MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI 'SUGU' AMEHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI MITANO


Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imewatia hatiani mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga na kuwahukumu kifungo cha miezi mitano jela kila mmoja.



Hukumu hiyo imetolewa leo Februari 26,2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Michael Mteite.

Sugu na Masonga wamehukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais  wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30, mwaka wa jana. eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment