NA, FARID SAIDY
MOROGORO
24/08/2017
Watu watatu wamefariki Dunia huku wengine 29 wakijeruhiwa, baada ya daladala waliyokuwa wakisafiria kugonga Treni ya abiria iliyokuwa inatokea bara kwenda Dar es salam katika eneo la Tanesco Manispaa ya Morogoro, huku idadi hiyo ya Majeruhi wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa Shule za Sekondari za Tushikamane na Mji Mpya.
Kwa mjibu wa Mganga mfawidh wa hospitali ya mkoa wa Morogoro DR Francis Semwene amethibitisha kupokea majeruhi hao 31 huku watatu wakifariki dunia ambao wawili na wanafunzi na mmoja akiwa bado hajulikani na wengine 28 wakiendelea Matibabu.
kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Ulrich Matei amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva aliyekuwa anaendesha daladala ambayo ilikuwa inatokea mjini kwenda Kihonda kuover take gari nyingine bila kuangalia mbele hatua iliyoplelekea kuivamia treni hiyo ya abiria iliyokuwa inatokea mkoani Kigoma kwenda Dar es Salaam .
Majeruhi wa ajali wanendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa morogoro huku dereva wa gari hiyo aina ya coster yenye namba za usajili T 438 ABL anashikiliwa na jeshi la Polisi baada ya kusababisha ajali hiyo na kutaka kukimbilia pasipojulikana ndipo wananchi wenye hasira walipomkamata na kuanza kumpiga na ndipo aliposaidiwa na polisi.
MWISHO:
No comments:
Post a Comment