Na, Omary Hussein, Morogoro
Mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Morogoro, kwa mara nyingine imeshindwa kutoa dhamana kwa Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Peter Lijualikali wa Kilombero pamoja na Suzani Kiwanga wa Mlimba na washtakiwa wengine 34 wa Chama hicho, baada ya kutokea mvutano wa kisheria baina ya upande wa Mawakili wa Serikali na ule wa utetezi, juu ya kiapo kilichowasilisha na Serikali cha kupinga washtakiwa hao kupatiwa dhamana, hatua iliyopelekea Hakimu Ivan Msaki, kuhairisha tena kesi hiyo hadi Desemba 6, watakapojadili tena kiapo hicho.



